Kilio Changu Mwajiriwa
Kwa kweli nina hasira, kwa yale unayotenda Wewe ulo na ajira, mesahau ya kalenda Wanipa chache mshara, uso fika siku kenda Nimechoka na kuimba, nilipe na nitaenda Mwezi umekamilika, hadi lini tasubiri? Mwajiri waajibika, waniumiza kisiri Hu ni ukweli hakika, moyoni waniathiri Nimechoka na kuimba, nilipe na nitaenda Nazivunja zangu sera, nizokuwa nimetenga Nipe wangu mshahara, labda jumba tajenga Nikuwapo na subira, waniona mi mjinga Nimechoka na kuimba, nilipe na nitaenda Wewe wacha zako pupa!,