SAFARI YA AJABU


2023/07/30 22:12
Follow

Ni hadithi inayomzungumzia mzee aliepitia mauza uza katika safari yake

SAFARI YA AJABU

Katika Kijiji Fulani bwana mmoja alipanga safari ya kwenda kumtembelea binamu yake aliyekuwa wilaya ya pili kutoka mahali alipokuwa akiishi.

Kutokana na wazo la safari yake, usiku wa kuamkia safari hakupatwa na usingizi kwani alikuwa na shauku ya safari ile. Alilala mpaka saa tisa usiku lakini usingizi hakupa.

Ilivyotimu saa kumi na nusu arufajili aliamua Bora aende akasubirie gari bara barani kwani magari yalikuwa yakitokea ng'ambo ya pili kutoka Kijiji chao.

Alifika bara barani na baada ya dakika Tano aliona gari linakuja na konda akashuka na kumuuliza, "Mzee unaelekea wapi?"

Alijibu 'naenda mkonzye" .

"Haya panda twende, kuna siti pale kati pita ukae". Konda aliongea huku akitoa maelekezo

Mzee akapita mpaka alipoelekezwa na kuketi. Safari ya mzee kuelekea Mkonzye ikaanza.

Walisafiri kwa muda wa nusu saa yaani tangu saa 10 na dakika 35 mpaka saa 11 na dakika 5. Ndipo mzee alipohisi kama anatoka usingizini na mara alipogutuka alishangaa kuona bado yupo pale pale aliopopandia gari muda wote ule.

Aliamua kujisachi mfukoni kuona kama alishalipa nauli na ajabu kweli alikuwa ameshakwisha kumpa nauli yule konda.

Mzee alishangaa na kujiuliza pekee yake, "ni nini hiki mbona siyo kawaida?"

Alichukua maji na kunawa uso japo aone labda atakuwa usingizi ni ndoto tu imemchanganya. Bado majibu yalikuwa Yale Yale kuwa hayupo kwenye gari ila pale pale aliopopandia gari. Alijaribu kuzigeuza fikra zake japo zione kama alikuwa ndotoni na hakuwa safarini.

Aliamua kupotezea na kujisemea " hamuna shida, nitasubiri gari jingine hapa hapa na kama ile ni ndoto bas buana isinipotezee muda kuifikiria".

Baada ya muda kweli gari likawa limefika kwa mara nyingine.

Alishuka konda na kumuambia. " Mzee gari limejaa hili, unauwezo wa kusimama japo kwa muda wakishuka hawa wa njiani ukae?"

Mzee alijibu, "bila shaka kijana".

Aliingia na kusimama, kulikuwa na kelele nyingi kwenye ile gari watu wakiongea huku na kule. Safari ikaanza kwa mara nyingine tena. Gari ilikuwa ikikimbia sana na kwakuwa bara bara ilikuwa ni ya kijijini, walipita mapori na mapori. Walivyotembea umbali wa kilometer 40, Mzee alishangaa kuona kwenye ile gari yuko peke yake na Wala kelele za wale watu wengine hakuna.

Uvumilivu ukamshinda, kwa hofu mzee akaanza kuita "konda konda konda".

Hapakuwa na mtu aliyekuwa akiitikia. Aliamua kusogea mbele akielekea kwenye mlango wa kutoke, alivyochungulia upande wa dereva alishangaa kuona dereva hayupo na wakati huo gari linaendelea kwenda.

Alihamaki kwa mshangao huku mwili ukimtetema. Aliushika mlango na ghafla gari lilisima mlango ukafunguka.

Alitoka nje ya lile gari na gari likaendelea kuenda.

Baada ya kumuacha kidogo, alishangaa kuona watu kwa mbali wakiwa kwenye lile gari. Alipigwa na butwaa, ikiwa inaelekea saa 12 na dakika 45 asubuhi.

Alishindwa kuvumilia na kuhisi labda aliamka muda ambao haukuwa sahihi, yaani ameamka muda ambao hakupaswa kuamka na kusubiria magari bara barani.

Aliamua kutembea kwa miguu, japo avute muda mpaka ifike saa Moja asubuhi.

Share - SAFARI YA AJABU

Support this user by sending bitcoin - Learn more

Follow

0 comments

Be the first to comment!

This post is waiting for your feedback.
Share your thoughts and join the conversation.