𝐮𝐣𝐮𝐦𝐛𝐞 𝐦𝐳𝐢𝐭𝐨 𝐤𝐮𝐭𝐨𝐤𝐚 𝐤𝐰𝐚 𝐦𝐚𝐫𝐞𝐡𝐞𝐦𝐮


Bongo Burudani2022/08/11 21:35
Follow

𝐩𝐚𝐭𝐚 𝐡𝐚𝐝𝐢𝐭𝐡𝐢 𝐳𝐚 𝐤𝐮𝐬𝐢𝐬𝐢𝐦𝐮𝐚 𝐤𝐮𝐩𝐢𝐭𝐢𝐚 𝐬𝐢𝐦𝐮 𝐲𝐚𝐤𝐨 𝐦𝐜𝐡𝐨𝐧𝐠𝐨 𝐛𝐨𝐧𝐠𝐨 𝐛𝐮𝐫𝐮𝐝𝐚𝐧𝐢 𝐧𝐚 𝒄𝒉𝒊𝒎𝒌𝒉𝒂𝒏 𝒎𝒂𝒔𝒕𝒐𝒓𝒚

SIMULIZI YA BARUA YA MSHANGAO

By 𝐜𝐡𝐢𝐦𝐊𝐡𝐚𝐧 𝐦𝐚𝐬𝐭𝐨𝐫𝐲

BARUA YA MSHANGAO ni simulizi fupi ya kusisimua iliyotungwa na mtunzi mahiri hapa nchini alimaarufu 𝐜𝐡𝐢𝐦𝐊𝐡𝐚𝐧 𝐦𝐜

.

karibu kusoma ukurasa huu wa BARUA hii ya MSHANGAO ilio andikwa na MAREHEMU JACKSON kwenda kwa kaka yake mpendwa JONHSON, NI BARUA iliobeba hisia na simanzi nzito za JACKSON, kijana ambaye alitengwa na familia yake kwa sababu ya wimbi zito la mapenzi alilopata kutoka kwa aliyekuwa mpenzi wake kwa JINA MAUA.

Mpendwa JONHSON!!!

Ni matumaini yangu kuwa humzima wa afya njema. Nimeamua kukuandikia waraka huu mfupi kukupongeza kwa kupiga hatua ambayo watu wengi wameshindwa kuifikia.mpendwa kaka nimejaa na mshangao sana na sielewi kwanini Dunia imekuwa ni sehemu iliyotanda wingu la USALITI namna hii,ndio maana najiuliza uliyonayo kwako ni ndoa au ndoano?.

JONHSON Nakuomba uipokee barua hii kama sehemu ya zawadi yangu kwako,kwani nimeshindwa kuhuzuria sherehe Ya ndoa yako kama ambavyo baadhi ya wetu walihitaji na kudhamilia kutohuona uwepo wangu harusini hapo .

Nilipokuwa kambini nilifurahi sana uliponitaarifu kuwa unataka kuoa,nilishangilia sana kwa kujua kuwa ukianza wewe kuoa na mimi nitamalizia, loooh bila kujua unataka kumposa Maua!!! wakati wewe ukiwa nje ya nchi mimi niliomba likizo fupi ilikuhuzulia siku yako ya kumposa niseyemzania, kumbe ulimposa shemeji yako!!!!.mara baada ya kuwasili nyumbani na kuelezwa utakaefuganae ndoa siku hiyo hiyo nilimfuata maua ilinipate kujua ukweli na uhalisia wa jambo hilo,lakini cha ajabu na kushangaza nilipokelewa kwa kukanwa na kunifukuza kama mtu asiye nijua.

Najua ulihuzunika sana uliposikia nimefanya vurugu siku ya kumposa MAUA, maua ambaye kwasasa amekua ni mke wako wa ndoa. mpendwa kaka yangu ningependa uelewe kuwa, zilikuwa si vurugu kama ambavyo uliambiwa,bali ilikuwa ni harakati yakudai haki yangu yamsingi iliyotolewa na kutupwa mbali kwa sababu yako.harakati ambayo ilinifanya nichukiwe na wazazi walionizaa hata kutengwa na familia iliyo nilea,

elewa kuwa si kwa sababu ya mafunzo ya jeshi nilio nayo ndio yalionifanya nivuruge mahari uliomposa maua,wala si wivu na maumivu yamapenzi kama ambavyo ilizaniwa.bali ni kiumbe changu ambacho maua alikitoa na kukiua bila hatia ili tu aweze kuolewa nawe,lakini sasa ndoa yenu imetimia na kubarikiwa si kwa wazazi tu bali hata jamii inatambua huyo ni mkeo wa ndoa.kwangu sikurahumu ka jambo ambalo hukulijua

Lakini Maua!!, maua!!,Nakueleza ukweliii Maua ni ua nililolijali na kulitunza kwa muda mrefu japo amekuficha siri hiyo.Maua ni msichana pekee niliyempenda katika hii dunia.Maua aliniahidi mambo mengi sana, nafahamu haukujua hayo, labda kwa sa babu ya safari zako za mara kwa mara nje ya nchi.pia hata wazazi wetu hawakufanikiwa kujua jambo ilo kwa sababu ya siri nzito niliyoificha wakati wa mahusiano yetu.

Maua ambaye alinifanya ni katishe ndoto zangu za kuendelea na masomo mara baada ya kuonja penzi lake zito.ndiye maua aliezima ndoto zangu za kuwa na familia iliyo na upendo na furaha tere.siwezi sema nitampata mwingine atakae nipenda,kwani sasa yale yote yamebakia kuwa historia.

Nikweli waswahili husema kizuri kula na nduguyo lakini maua si ua salama kaka. inawezekana ni pesa na utajiri ulionao ulimfanya ashawishike na kukubali kuolewa na wewe japo ni shemeji yake, nakushindwa kunivumilia mimi niliye jiunga na jeshi ilikuijenga kesho aliyoniongopea yenye furaha ya mapenzi na raha ya maisha,nakuhurumia sana kaka yangu. japo nilijaribu kupaza sauti kukemea haya yaliotokea nilipuuzwa na kuonekana niliyeasilika na kuchanganyikiwa na mafunzo ya jeshini

Kaka kwa sasa hali yangu si nzuri kiafya,hii ni kutokana na ajari mbaya nilio ipata siku nilio kuwa natoka nyumbani kurejea kambini mara baada ya kumaliza likizo yangu fupi.nilishindwa kutoa taarifa nyumbani kwani hakuna anayenijali wala kunithamini mdogo wako, sasa siwezi kusimama wala siwezi kukaa. nimelala kwa muda mrefu huku maumivu mazito yakinihandama,hata miguu uliyozoea kuiona uwanjani ikipiga chenga na kufunga magori kama mvua kwa sasa hutoiona tena,imezikwa angali nikiwa hai.

Hamakweli kikulacho kiinguoni mwako, haya yote yanayonisibu ni kwa sababu ya MAUA!! lakini kama ameweza kunizuru mimi niliekuwa nae kwa muda mrefu atashindwaje kukuzuru wewe ambaye amekupenda kwa sababu ya pesa?siamini kama maua ni mshirikina lakini ulemavu nilioupata siku niliokuwa nalejea kambini ni wazi kuwa yeye alikua ni chanzo cha ajari ile, kwani licha ya kuniahidi kunifanyia kitu ambacho kitakacho nifanya nisimsahau katika maisha yangu, yeye ndiye aliyenitokea katikati ya barabara na kufanya gari langu lilokuwa kwenye mwendo kasi lipoteze mwelekeo kabla ya kupolomoka na kugonga mwamba katika makolongo ya Mlima kitonga.

Maua licha ya kumuangamiza mwanangu kwa kutoa mimba nilioiacha ikiwa na miezi mitatu. leo ameniangamiza na mimi!!!.iko wapi ahadi yetu ya kuishi pamoja mpaka kufa,leo ameweza kuliangamiza ua na boga lake,kwa hakika siwezi kupona tena. kaka mdogo wako uhai wangu unahesabika!! ni siku chache tu zimebaki kabla ya kuwaacha wapendwa wangu katika ulimwengu huu,

Naomba uwasihi sana baba na mama kunisamehe mtoto wao. na punde tu watakapo pata waraka huu nawaomba muambatane kwa pamoja kuja kuuchukua mwili wa ndugu yenu, kwani mimi ni miongoni mwa damu ya SAMSON Mzee wa familia yenu.Nnawasihi sana msije kuutenga mwili wangu kama ambavyo mlinitengwa enzi za uhai wangu na kufanya nikazikwa huku ughaibuni kama mtu mlowezi. Naomba umsalimie mziwanda wetu ANETH ,mdogo wangu kipenzi ambaye sijui na muacha katika maumivu gani, Mwambie anikumbukapo aitazame mbalamwezi ng'avu ataniona tena katika tabasamu alilonifundisha. mimi sina mengii nawatakia maisha yenye furaha na amani.Mimi nimetangulia tu wakati ukifika nanyi mtakuja huku nilipo

Ni wako JACKSON SAMSON KUMBO

@𝐜𝐡𝐢𝐦𝐊𝐡𝐚𝐧 𝐦𝐚𝐬𝐭𝐨𝐫𝐲

Follow

Support this user by bitcoin tipping - How to tip bitcoin?

Send bitcoin to this address

0 comments